New titles published weekly — explore the Discussion Publishers catalogue
Discussion Research

East African Journal of Swahili Studies · 2025

Uchambuzi wa Stailikia za Ufupishaji katika Mtandao wa WhatsApp

Winifrida Moshi

Abstract

Utafiti huu umeshughulikia “Uchambuzi wa Stailikia za Ufupishaji katika mtandao wa WhatsApp na mchango wake katika ukuaji wa lugha ya Kiswahili. Utafiti huu umetumia muundo mseto, wa kitakwimu na wa kimaelezo. Sampuli iliteuliwa kwa kutumia mbinu ya usampulishaji nasibu sahili ili kuweza kupata data za utafiti. Utafiti huu ulifanyika mkoani Mwanza katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino kilichopo Wilaya ya Nyamagana katika jiji la Mwanza. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ni Nadharia ya “Uchanganuzi Tahakiki Usemi”. Utafiti huu ulikusanya data kutoka uwandani, mbinu iliyotumika kukusanya data ni mbinu ya dodoso. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa, staili ya ufupishaji katika mtandao wa WhatsApp inayotumiwa na watu wengi ni ya kudondosha baadhi ya herufi katika neno, kwani ni 77% ya watafitiwa wote waliojibu swali hili hudondosha herufi wanapofupisha maneno. Pia, matokeo yalionyesha kuwa mtandao wa WhatsApp ni jukwaa ambalo limesaidia kukua na kuenea kwa Kiswahili miongoni mwa watumiaji kwa kuwa mtandao huu hutumiwa na watu mbalimbali. Mapendekezo yanatolewa kwa Taasisi inayochunguza na kukuza Kiswahili kuvisanifisha vifupisho vya maneno vinavyotumika katika mitandao ya kijamii kwani ni vigumu sana kudhibiti matumizi ya vifupisho kwa kuwa mawasiliano ni uhuru wa mtumiaji na anawasiliana kwa staili anayopenda yeye. Kwa watumiaji wa lugha ya kiswahili, wanapaswa kutofautisha matumizi ya lugha rasma na lugha ya kawaida ili kuepuka kuchanganya matumizi hayo kwa kuwa watumiaji wengi wanapofupisha au kuandika maneno kimtandao hawafuati sifa za konsonanti na vokali wao huandika konsonanti mbili zikifuatana au konsonanti peke au vokali pekee. Wanaunda na kuandika maneno kulingana na jinsi yanavyokaribiana au kuhusiana kisauti. Wakati mwingine wanaacha silabi fulani katika neno kwa sababu wao wanaamini kuwa maana ya neno huweza kuwakilishwa bila kuwepo kwa fonimu fulani.

How to cite

Winifrida Moshi (2025). Uchambuzi wa Stailikia za Ufupishaji katika Mtandao wa WhatsApp. East African Journal of Swahili Studies. https://doi.org/10.37284/jammk.8.3.4069

Republished on Discussion Research from the global Crossref scholarly index with full credit to the original authors and East African Nature and Science Organization. Licence: http://creativecommons.org/licenses/by/4.0